Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza matokeo ya ubunge katika majimbo ya Mkoa wa Singida ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeonekana kung’aa.

Katika jimbo la Singida Magharibi, Msimamizi wa uchaguzi amemtangaza Kingu Elibarick wa CCM kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo baada ya kupata kura 25,102 akimuacha mshindani wake mkuu, Marico Alute wa Chadema.

Kingu Elibarick

Kingu Elibarick

Jimbo la Singida Mahariki limerudi kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Tundu Lissu wa Chadema ambaye msimamizi wa uchaguzi amemtangaza rasmi baada ya kupata kura 24,874 akifuatiwa na Jonathan Andrea wa CCM aliyepata kura 18,393.

Msimamizi huyo wa uchaguzi pia alimtangaza Allan Joseph wa CCM kuwa mbunge mteule wa jimbo la Iramba Mashariki kwa baada ya kumshinda mpinzani wake mkuu Oscar Kapalali wa Chadema. Alan Joseph alishinda kwa kishindo akipata asilimia 70.69.

Imekuwa heri kwa waziri wa maliasili na utalii, Lazaro Nyalandu baada ya kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini kwa mara nyingine.

Twiga Kucheza Na Malawi Novemba 7
Song Kupanga Mikakati Dhidi Ya Taifa Stars