Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza kuyafuta matokeo ya mitihani ya Darasa la saba kwa shule za msingi zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Chemba, pamoja na baadhi ya shule katika halmashauri ya Kondoa, Kinondoni, Mwanza jiji na Ubungo kwa kosa la kuvujisha mitihani ya darasa la saba ikiwa ni kinyume na taratibu na kanuni za mitihani nchini.

Miongoni mwa shule zilizokumbwa na kadhia hiyo ya kufutiwa matokeo ni Shule ya Msingi Hazina na New Hazina zilizopo wilaya ya Chemba, Shule ya Msingi Kisiwani, iliyopo Ubungo, Shule ya Msingi Kondoa iliyopo Halmashauri ya Kondoa, pamoja na Shule ya Msingi Alliance na New Alliance zilizopo halmashauri ya Mwanza jiji.

Uamuzi huo umechukuliwa leo katika mkutano maalum wa 125 uliofanywa na Baraza la mitihani Tanzania jijini Dar es salaam ambapo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) Charles Msonde amesema.

“Kufuatia kuvunjwa kwa kanuni za mitihani baraza limeamua kufuta matokeo ya kumaliza shule ya msingi ya halmashauri ya Chemba pamoja na shule ya Hazina na Kinondoni, Anyindumina na Font of Joy za Ubungo, Alloiance na New Alliance ya Mwanza jiji pamoja na Kondoa Integrity ya Kondoa Mjini, na watahiniwa wa mtihani hiyo watairudia tena oktoba 8 na tarehe 9 wiki ijayo. Amesema Charles Msonde.

Aidha baraza hilo limefuta vituo vya mitihani kwa shule nane ambazo zilihusika katika uvujishaji wa mitihani hiyo sambamba na kupendekeza kuondolewa kwenye nafasi za ajira kwa baadhi ya maafisa elimu kata na wilaya waliohusika kwenye udanganyifu huo.

Shule zote za msingi halmashauri ya chemba dodoma na shule saba binafsi zimefutiwa mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi baada ya kubainika kuiba mitihani hiyo na kuwapa majawabu ya maswali watahiniwa ambapo watarudia mitihani hiyo septemba nane na tisa mwaka huu huku watuhumiwa wote wakiendelea kushikiliwa.

 

John Mikel Obi aomba kuachwa Super Eagles
Simba SC yawapongeza na kuwaondoa hofu mashabiki