Wabunge watatu nchini Kenya wametaka wataalam wa kimataifa wafanye ukaguzi wa kina kuhusu matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2017.

Wabunge hao wamemtaka Waziri wa Elimu nchini humo, Fred Matiang’i ajiuzulu katika kipindi cha wiki moja, na kama hatafanya hivyo watachukua hatua ya kuwasilisha muswaada Bungeni wa kumuondoa madarakani wakati Bunge litakapoanza shughuli zake.

Aidha, wamesema kuwa wamemwandikia barua Spika wa Bunge la nchi hiyo, Justin Muturi awaite ili waweze kujadili ukweli kuhusu matokeo ya mitihani hiyo wakimtuhumu Waziri wa Elimu kwa kutoa matokeo ambayo hayajafanyiwa marekebisho yoyote, jambo lililosababisha wanafunzi wengi kufeli.

Hata hivyo, zaidi ya asilimia 80 ya wanafunzi hawakuweza kufikia alama ya C+ na juu ya hapo katika mtihani wa kidato cha nne 2017.

TFF yakanusha zuio la michuano isiyo rasmi
Video: Mtoto aliyefanyiwa operesheni 10 asafirishwa kwenda India kwa ajili matibabu