Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu wa Polisi, SP Solomon Mwangilo amewataka madereva na wamiliki wa matrekta Mkoa wa Arusha, kufuata sheria za usalama Barabarani Ili kupunguza na kumaliza ajali katika Mkoa huo.

Mwangamilo ameyasema hayo hii leo October 20, 2022 wakati akizungumza na Madereva na wamiliki wa Matrekta katika katika kata ya Kikatiti wilaya ya Arumeru, na kusema takwimu zinaonyesha kuwa ajali nyingi zinasabibishwa na vyombo hivyo, kwa kukosa viakisi mwanga.

Amesema, “Kuna ajali nyingi ahasa maeneo ya kikatiti, na hatari nyingi zinasababishwa kwa trekta kutokuwa na viakisi mwanga au reflector na nimetoa mwezi mmoja muwe mmeweka na taa pia ziwepo za nyumba na mbele na atakayekiuka ikianza operasheni ambayo haitamgusa dereva tu ni hadi mmiliki kwa kushindwa kutii sheria.”

Baadhi ya madereva na wamiliki wa vyombo hivyo, wamepokea maelekezo hayo na kwamba watayafanyia kazi kwa muda muafaka kwani elimu hiyo imewaondoa katika sintofahamu waliyokuwa nayo hasa katika uwekaji wa viakisi mwanga.

Magari matatu yagongana, mmoja afariki
Ahmed Ally aipiga kijembe Young Africans