- Wizi Benki ya Pennsylvania
Rekodi za wizi mkubwa unaoshika nafasi ya kwanza Duniani ni ule uliofanyika katika benki nchini Marekani eneo la Philadelphia Agosti 31, 1798. Pesa zilizoibiwa zilikuwa ni Dola 162,281 kiasi ambacho ni kikubwa kuwahi kutokea katika wizi uliowahi kufanywa Duniani.
- Wizi wa Sanaa ya Mona Lisa
Kuna picha maarufu ya Leonardo da Vinci, Mona Lisa, yenyewe ilihifadhiwa katika Makumbusho ya Louvre huko Paris. Ilikuwa ni moja kati ya ya kazi kubwa zaidi za sanaa katika historia ya Ulimwenguni lakini Agosti 21, 1911, picha hiyo iliibwa.
- Wizi wa Kazi za Sanaa
Kati ya mwaka 1933 na 1945, Serikali ya Kisoshalisti ya Kitaifa ya Ujerumani ilikuwa katika harakati za kunyakua kazi za sanaa za Wayahudi na mataifa ambapo urithi wa kitamaduni ulihusiana na hamu ya Hitler ya kuanzisha jumba la kumbukumbu kubwa la sanaa huko Austria.
Vita vilipoanza mnamo 1939, timu zilitumwa Ufaransa, Ubelgiji, Uholanzi na nchi zingine kuunda hesabu ya kazi zinazohitajika, ambapo haikuwezekana hata kukadiria jumla ya thamani ya vipande vya kuibwa.
Hivyo Mamlaka ya Ujerumani ililinganisha picha 1,100 za uchoraji katika jumba la zamani la sanaa huko Munich, na zililiibwa na Wanazi mwaka 2011 huku thamani ya kazi hizo iliyoibwa ikikadiriwa kuwa ni zaidi ya Dola 1 bilioni.
- Wizi katika Treni
Treni ya Royal Mail ya huko Buckinghamshire nchini Uingereza, ilikuwa imebeba dola milioni 3.9 lakini kuna wahuni waliziba mwaka wa 1963, na wizi huo ukawa ni mojawapo ya wizi maarufu zaidi nchini Uingereza ambao ulipangwa kwa uangalifu kwa miezi kadhaa.
Wezi hao, walifanikisha tukio hilo baada ya kubadilisha ishara za reli za kusimamisha treni na kufanya wizi huo kiulaini na kutokomea kusikojulikana huku wahusika na watumishi wakibaki wameduwaa.
Ingawa pesa hizo hazikupatikana, lakini wengi wa washiriki wa genge hilo baadaye walinaswa na Polisi mmoja baada ya mwingine.
- Wizi wa Dunbar
Agosti 6, 2009 Aman Kassaye na mshirika wake walifika Graff Jewellery kwenye barabara ya New Bond huko London na kuwaliwalazimisha wafanyakazi kufungua madirisha kisha wakaiba jumla ya almasi zenye thamani ya dola milioni 65 na vito vingine vya thamani na tukio hili pia kuiingizwa kwenye rekodi za Dunia.