Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameiagiza Halmashauri ya Mji wa Geita kuhakikisha wanasimamia vema Mpango kabambe wa Mji wa Geita 2017-2037 bila kuruka hatua za utekelezaji.
Naibu Waziri Mabula ameyasema hayo wakati akizindua mpango huo katika Halmashauri ya Mji huo.
Amesema kuwa Mkoa wa Geita umebahatika kuwa na shughuli nyingi zikiwemo za uchimbaji dhahabu na kuufanya Mkoa huo kupewa jina la ‘mji wa dhahabu’ huku akisisitiza fursa ya dhahabu kutumika vizuri ili kuleta mapinduzi ya haraka ya kiuchumi na kijamii katika mji huo.
Aidha Dkt. Mabula, amesema Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Wizara ya Madini inaangalia namna bora ya kuwatambua wachimbaji wadogo wote ili waweze kupata fursa ya kumililkii maeneo yao kwa kuwa na hati ya umiliki wa ardhi.
‘’Wachimbaji wadogo wana leseni za uchimbaji madini lakini mgogoro huku juu ni mkubwa sana kwa sababu tu hawajatambulika,” Amesema Dkt Mabula.