Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman amewataka Wasimamizi wa Sekta ya Ardhi na Mazingira nchini, kuweka mipango maalum na sahihi ya kuyanusuru maeneo yote yaliyoathirika kwa maporomoko ya maji na matumizi ya Binadamu ukiwemo ujenzi na uchimbaji wa mchanga, ili kuzuia athari kutokea.

Othman ameyasema hayo alipotembelea mashimo ya mchanga ya Donge Muwanda Kaskazini ‘A’ Unguja pamoja na maporomoko ya Masingini katika Shehia ya Mtoni Chemchem Wilaya ya Magharib A Unguja, akiwa kwenye ziara maalum za kuangalia athari mbalimbali za maeneo hayo.

Amesema, Zanzibar inaendelea kuwa na miradi mikubwa ya uwekezaji na mahitaji ya rasilimali ya mchanga inaendelea kuongezeka sambamba na kuwepo athari za kimazingira jambo linalohitaji mipango sahihi katika matumizi ya raslimali ya ardhi iliyopo.

Aidha, Othman amesema ardhi iliyopo Zanzibar ni ndogo na ina ongezeko la mahitaji makubwa lakini ni lazima kila eneo la ardhi lililopo litumike kwa tija kwani ardhi ni miongoni mwa rasilimali zenye thamani kubwa na matumizi ya rasilimali za ardhi katika miradi ya kimaendeleo yataendelea kuwepo.

Tanzania kushirikiana na IFAD miradi Sekta ya Kilimo
Tushirikiane kuwahudumia Wananchi - Prof. Ndalichako