Msanii wa muziki wa bongo fleva ‘Hitmaker’ wa Iokote Maua Sama kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amefunguka na kusema hawezi kuzisahau siku 10 alizozipitia pindi akiwa mahabusu.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Maua amedai kuwa zilikuwa ni siku ngumu ambazo hajawai kuzipitia katika maisha yake.

Maua Sama alikamatwa na Polisi wiki mbili zilizopita kwa tuhuma za kuidhihaki pesa ya Tanzania kwa kupost video inayoonesha watu wakizichezea pesa za kitanzania.

Tarehe 25 Septemba Maua Sama na mtangazaji wa CloudsFm Soudy Brown waliachiwa  kwa dhamana.

Gareth Southgate kusaini mkataba mpya
Video: Mgaya awapiga dongo wapinzani, ataka washindane kwa hoja