Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, amesema tangu ateuliwe kuongoza Wizara hiyo Kuna mambo mawili yanayomnyima usingizi ikiwemo mauaji yanayotekelezwa na baadhi ya watu kwenye jamii pamoja na baadhi ya askari kufanya vitendo kinyume na maadili.
Waziri Masauni amesema hayo baada ya kushuhudia onesho la medani za kivita lililoandaliwa na askari wanaotarajia kuhitimu kozi ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi katika kambi ya kivita ya Kambapori iliyopo wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa, Jeshi la Polisi nchini limejipanga kukabiliana na matishio mbalimbali ikiwemo wa kutumia silaha za moto na kwamba hakuna mhalifu atakayefanikiwa kutekeleza tukio la kihalifu.
Aidha, IGP Sirro amesema kuwa, kamwe Jeshi la Polisi alitomvumilia askari yeyote atakayekwenda kinyume na kanuni na taratibu za Jeshi hilo.