Watu wasiopungua 50 wameuawa katika shambulio lililofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu, katika Jimbo la Sahel lililopo kaskazini mwa nchi ya Burkina Faso.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali ya nchi hiyo, Lionel Bilgo amesema tukio hilo ni baya kuwahi kutokea katika moja ya mapigano ya umwagaji damu, tangu yalipotokea mapinduzi ya Kijeshi mwezi Januari mwaka huu.

“Jeshi kufikia sasa limepata miili 50 baada ya kijiji cha Seytenga kushambuliwa usiku wa kuamkia Jumamosi Juni 11, 2022 na idadi ya vifo huenda ikaongezeka,” amesema Bilgo alisema, akiongeza kuwa idadi ya watu “huenda ikaongezeka.”

Amesema kabla ya mkasa huo Wanajeshi 11 waliuawa siku ya Alhamisi ya Juni 9, 2022, na kusababisha operesheni ya kijeshi ambayo ilipelekea vifo vingine vya wanajihadi 40 kutokana na mapigano.

“Umwagaji damu wa mwishoni mwa wiki ulisababishwa na vitendo vya kulipiza kisasi kwa jeshi ambalo linaendelea na operesheni za kuwaondoa waasi ambao wanajiita wanamgambo wa jihad japo nchi imepigwa lakini bado Jeshi litafanya kazi yake,” alisema Bilgo.

Mashirika ya kibinadamu katika eneo hilo yanasema karibu watu 3,000 walikuwa wakitafuta hifadhi katika miji ya jirani, baada ya kukimbia kutoka kijijini kuepuka machafuko hayo ambayo yamesababisha uharibufu wa mali na vifo.

Jimbo hilo la Sahel ambalo halina Bahari liko chini ya uasi kwa miaka saba, ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 na kuwalazimu takriban watu milioni 1.9 kuyakimbia makazi.

Bilgo anasema “mashambulizi mengi yameathiri upande kaskazini na mashariki mwa nchi na tunaambiwa yanaongozwa na wavamizi tunaowaoshuku kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda au kundi la Islamic State.”

Shambulio hilo ni mojawapo ya matukio ya umwagaji damu mkubwa kuwahi kutokea tangu jeshi liliposhika madaraka mwezi Januari, baada ya kukasirishwa na kitendo cha viongozi kushindwa kuondoa uasi uliomwondoa madarakani Rais Roch Marc Christian Kabore.

Ruzuku ya TASAF yamuweka kikaangoni mtendaji wa kijiji
Singida Big Stars yamakataa Ditram Nchimbi