Mauaji ya kutumia silaha yanaendelea kujitokeza wilayani Rufiji mara baada ya kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amiri Chanjale mkazi wa Umwe ,tarafa ya Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani kuuawa kwa kupigwa risasi kichwani na watu wasiojulikana.
Mkuu wa wilaya hiyo, Juma Njwayo amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo wakati marehemu akiwa amepumzika nyumbani kwake.
Amesema kuwa watu hao walifika nyumbani kwa marehemu na kuingia ndani kisha kumfyatulia risasi ya kichwa hali ambayo ilimsababishia maumivu makali ambayo yalipelekea kupoteza uhai na watu hao kutokomea kusikojulikana.
“Jeshi la polisi bado linaendelea na kazi yake ya kuwasaka wauaji na mtandao wao wote, hivyo niwatoe hofu wananchi kuwa kila kitu kinaanza taratibu, na Serikali itashinda kwani hakuna linaloshindikana,”amesema Njwayo
Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Onesmo Lyanga, amesema kuwa polisi bado inaendelea na kazi yake usiku na mchana kuwasa na kuhakikisha wanaukamata mtandao wote unaohusika na mauaji hayo.
 Hata hivyo, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amewatoa hofu wananchi wa maeneo hayo na kusema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na operesheni yake ya kuhakikisha mtandao wa wahalifu hao unatokomezwa.

Video: Madaktari kutoka India watua nchini kutoa huduma za kiafya
Korea Kaskazini Yadai Kunasa Njama za Marekani Kumuua ‘Kim Jong-Un’