Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Naphtali Ng’ondi amesema Serikali imefanikiwa kupunguza mauaji ya wazee nchini kutoka wazee zaidi ya 500 miaka mitano iliyopita, na mwaka 2019 mauaji 74 tu yaliripotiwa.

Aidha, amesema wameongeza idadi ya wazee wanaopatiwa huduma za afya bure na wameboresha vituo vya kuwatunza wazee nchini.

Maadhimisho ya siku ya wazee duniani yonayodhimishwa Oktoba 1 kila mwaka inayotambulika na Umoja wa Mataifa katika Azimio namba 45/106 la mwaka 1990

Siku hii ni mahususi kwa ajili ya kutambua Haki na Changamoto wanazokumbana nazo wazee katika jamii huku, Tanzania maadhimisho haya mwaka huu yaNafanyika kimkoa.

Papa Francis akataa kuonana na waziri wa Marekani
Tetesi: Guendouzi kurudi Ufaransa, Houssem Aouar kusajiliwa Arsenal