Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewataka viongozi wa Dini, makundi ya kijamii, wazee na makundi yote ya vijana mkoani humo kuendelea kutoa elimu ili kukomesha matukio ya mauaji yanayoendelea.
Rc Mrindoko ametoa agizo hilo kufuatia mauwaji yanayoendelea kutokea katika Mkoa wa Katavi ambapo kuanzia mwezi Januari hadi sasa watu 18 wameuawa kwa visa tofauti ikiwemo wivu wa mapenzi, visasi na tuhuma za kishirikina.
RC Mrindoko amesema kama Serikali wataendelea kuchukua hatua zinazostahili ili kudhibiti matukio hayo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika endapo yatatokea huku lengo ikiwa ni kuzuia kabisa matukio ya mauwaji.
“Watu kugombania mali, wivu wa kimapenzi,kugombania ardhi lakini na tuhuma za kishirikina watu wanatoana uhai,na wengine kutaka kupata mali bila kuifanyia kazi na huu tunasema unyang’anyi wa kutumia nguvu au wizi nao pia umechukua maisha ya baadhi ya binadamu ndani ya mkoa wa Katavi”,Amesema RC Mrindoko.