Ajira ya meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane, bado ipo shakani kufuatia mvutano unaoendelea kwenye vikao vya uongozi wa klabu hiyo, ambayo siku zote imekua ikihitaji mafanikio ya kutwaa mataji kwa haraka.

Zidane alianza kujadiliwa na kuwagawa viongozi wa juu, kufuatia matokeo ya kupoteza mchezo dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG) juma lililopita, kwa kufungwa mabao matatu kwa sifuri.

Taarifa mbalimbali zimekuwa zikielezwa kuhusiana na kipigo hicho na hali ya usalama wa kibarua cha Zidane huko Bernabeu, ambapo meneja wa zamani wa wababe hao wa Bernebau, Jose Mourinho, ambaye kwa sasa hana kazi aliripotiwa angerudishwa kuchukua mikoba.

Meneja wa Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino anapewa nafasi kubwa ya kumrithi mfaransa huyo, ambaye alikubali kurejea Santiago Bernabeu, miezi michache kabla ya msimu wa 2018/19 kufikia kikomo.

Kwa mujibu wa The Mirror, Pochettino ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kwenda kuchukua mikoba huko Bernabeu, wakiamini kwamba hata mshahara wake hautakuwa mkubwa sana, na inakadiriwa huenda akakubali kulipwa Pauni milioni 8.5 kwa mwaka.

Spurs ya Pochettino ilikuwa kwenye ubora wake msimu uliopita ikifika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufungwa na Liverpool huko Madrid, na mabosi wa Los Blancos wanaamini itakuwa vyema kama atakwenda kumbadili Zidane huko Bernabeu.

 

Tunda na Whozu watifuana
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 26, 2019