Kocha Mauricio Pochettino amethibitisha Chelsea inataka angalau wachezaji wawili wa kusajiliwa kabla ya dirisha la usajili kufungwa kutokana na nyota majeruhi waliopo.

The Blues tayari wametumia zaidi ya pauni milioni 320 msimu huu wa joto, lakini Pochettino anataka kuongezwa fedha zaidi huku orodha ya majeruhi ikiongezeka na wachezaji tisa wakikosekana.

Mykhailo Mudryk ndiye aliyekosekana hivi karibuni baada ya kupata tatizo dogo mazoezini wiki hii huku Carney Chukwuemeka akifanyiwa upasuaji wa goti Jumatatu na anatarajiwa kuwa nje kwa takriban wiki sita.

Mchezaji mpya, Romeo, Lavia hajaumia lakini hatacheza kwa kwa mara ya kwanza kwa wiki chache” akijaribu kupata utimamu na hiyo imechochea nia ya kuimarisha kikosi kabla ya Septemba Mosi.

Mmoja wa wachezaji wapya watakaowasili atakuwa ni kipa wa New England Revolution, Djordje Petrovic, ambaye anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kununuliwa kwa pauni milioni 14 huku Chelsea pia ikifikiria kumnunua Brennan Johnson wa Nottingham Forest na Mmarekani anayeichezea Arsenal, Folarin Balogun.

“Tunahitaji angalau kipa mmoja,” alisema Pochettino Alhamisi.

“Tuna walinzi chipukizi wenye vipaji, lakini wanahitaji muda. Tunahitaji zaidi na kisha tukazungumza kuhusu mchezaji mmoja mkabaji.

“Kama tunaweza kuongeza wasifu, sahihi, ndio, lakini sio kuleta wachezaji ili tuongeze mwingine. Wengi wao ni bahati mbaya,” alisema Pochettino.

“Nkunku na Carney au Fofana. Unawezaje kudhibiti? Sio juu ya mafunzo au mnafunzo kwa bidii au kidogo au sana au mbinu. Wakati mwingine hutokea.

Katwila asitisha mapumziko Ihefu FC
Singida Big Stars yaichimba mkwara JKU