Kocha wa Chelsea, Maurico Pochettino amesema kuwa kurudi Tottenham litakuwa jambo maalumu na la aina yake.

Chelsea leo Jumatatu (Novemba 06) itakuwa mwenyeji wa Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Tottenham Hotspur jijini hapa.

Pohettino anasema kuwa litakuwa jambo maalumu sana kurudi tena katika klabu uliyotengeneza kumbukumbu ya aina yake na timu hiyo wakati Chelsea itakaposafiri na kuifuata Tottenham.

Kocha huyo Muargentina aliifundisha timu hiyo kwa miaka mitano kabla ya kutupiwa virago mwaka 2019 na kuiongoza klabu hiyo kucheza fainali yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mapema mwaka huo.

Atarejea kwa mara ya kwanza katika klabu yake hiyo ya Kaskazini mwa London katika kipindi cha miaka minne akiwa na Chelsea kesho Jumatatu katika mchezo utakaoanza saa 2:00 usiku.

“Kwangu itakuwa siku yenye furaha kubwa,” alisema Pochettino, mwenye umri wa miaka 51.

“Tunafanya kazi, lakini wakati huohuo sisi nĂ­ binadamu na tunahisia pia.

“Kwa kweli ni jambo zuri kurudi katika eneo ambalo uliweka kumbukumbu kubwa na ya aina yake. Sitakwenda kulia. Huo ndio ukweli.”

“Wakati tunaondoka katika klabu kilikuwa kipindi kigumu lakini sasa tuna nafasi ya kurudi na kuangalia watu werngi ambao bado wanafanya kazi pale. Utakuwa wakati mzuri sana.”

Alipoulizwa kama kurudi tena kwa vinara hao Tottenham, ambayo inafikiriwa kuwa timu inayowania taji msimu huu kama atahisi sawa na kumuona mshirika wake wa zamani, Pochettino alitania: “Ni vigumu kwa sababu nina karibu miaka 32 na mke wangu na sijui kama nakumbuka kama niliwahi kuwa na mpenzi kabla.”

Kufuatia kuondoka Tottenham, Pochetino kocha wa zamani wa Espanyol alitua Paris St-Germain (PSG) mwaka 2021, ambako alitwaa mataji ya kwanza akiwa kocha kwa kushinda lile la Ufaransa 2021 na Ligue 1 2022.

Alirudi Ligi Kuu akiwa na mabingwa mara sita wa Uingereza, Chelsea Julai, akiwa na kibarua cha kuiimarisha Chelsea baada ya kumaliza katika nafasi ya 12 msimu uliopita.

Walimu waliosimamishwa warudishwe kazini - Dkt. Tulia
Idadi ya Watanzania wanaotembelea Hifadhi yaongezeka