Kiungo wa Young Africans, Zawadi Mauya amefunguka sababu iliyowafanya washindwe kutamba tena dhidi ya Simba SC kuwa ni kucheza pungufu ndani ya dakika 45.
Young Africans walimaliza mchezo huo wa Fainali Kombe la Shirikisho wakiwa pungufu, kufuatia kiungo kutoka DR Congo Mukoko Tonombe kuoneshwa kadi nyekundu, baada ya kumpiga kiwiko nahodha na mshambuliaji wa Simba SC John Bocco.
Mauya amefunguka suala hilo baada ya kikosi cha Young Africans kuwasili jijini Dar es salaam leo Jumatatu (Julai 26), kikitokea Kigoma.
“Mchezo ulikuwa mgumu na wa preshak kila upande ulitaka kupata matokeo mapema kwa upande wetu hatukulewa ushindi wa mwisho dhidi ya wapinzani tuliingia kwakujiamini tukihitaji ushindi lakini haikuwa rahisi wapinzani wetu walijipanga pia,” amesema.
Mauya amesema wao walikuwa bora na wapinzani wao walikuwa bora washukukuru kadi hawakuwa wazembe hivyo walihitaji heshima lakini kukosa kwao matokeo wamechukulia kama sehemu ya mchezo amewapongeza Simba kwa kutwaa taji hilo huku akiwaambia kuwa wakutane msimu ujao.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma, ulishuhudia Simba SC wakipata ushindi wa bao 1-0 lililogungwa na kiungo wa Uganda Thadeo Lwanga dakika ya 80.