Maveterani wa Jeshi la Marekani wanaounda kundi lenye watu zaidi ya milioni 2 wameanzisha harakati wakilitaka Bunge kuidhinisha bangi kuwa moja kati ya dawa za asili.

Wamelitaka Bunge hilo kutoa idhini hiyo ili kutoa fursa ya kufanyika kwa tafiti zaidi kuona kama bangi inaweza kutumika kama tiba sahihi kwa ajili ya magonjwa yanayotokana na msongo wa mawazo.

Kwa mujibu wa mtandao wa news.vice,  kundi hilo linalotambulika kama American Legion, ambalo ni kubwa zaidi nchini humo limepitisha maazimio ya kulitaka Bunge kuondoa bangi katika orodha ya dawa za kulevya yaliyo kwenye kundi la Heroin na madawa mengine.

Mwezi Agosti, Kitengo cha Dawa (Drug Enforcement Administration) nchini humo ilitupilia mbali rasmi maombi yaliyokuwa yakifanyiwa kazi kwa miaka mitano kuhusu kuondoa bangi katika orodha ya madawa ya kulevya hatari.

Ongeza thamani yako
Kumekucha: TFF Yataja Makundi Ligi Daraja La Pili