Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde, amesema anakusudia kuboresha sekta ya elimu katika mkoa wa Dodoma, ikiwemo kutatua changamoto mbalimbali zilizopo kwa lengo la kuongeza chachu ya ufundishaji na idadi ya ufaulu kwa wanafunzi.

Mavunde ameyasema hayo juzi, na kuwasisitiza wazazi kuhakikisha wanatumia fursa ya uwepo wa shule na vyuo vingi ndani ya jiji la Dodoma, kuwapeleka watoto shule kupata Elimu itakayowasaidia maishani hapo baadae.

Amesema ni vyema Walezi, Wazazi na jamii nzima ya Dodoma wakatumia fursa aliyoitoa Rais, John Magufuli ya elimu bure, kuwapeleka watoto wao kupata elimu ili waweze kunufaika na ujirani wa shule na vyuo mbalimbali zilizopo katika eneo lao.

“Tusiishie kujinadi tu kwamba Dodoma kuna vyuo vingi au shule nyingi, tunapaswa pia kuhakikisha watoto wetu wanatumia uwepo wa vyuo hivyo kikamilifu kwa kuwasomesha hapa wafaidike navyo,” Ameongeza Mavunde.

Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini amesema mkoa wake unazidi kupiga hatua katika sekta ya elimu, hivyo si vyema kwa wahusika hasa wazazi kuviona vyuo hivyo kama mapambo.

Amebainisha kuwa maeneo ambayo atayashughulikia ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za miundombinu, upungufu wa madarasa, ofisi za walimu na vitendea kazi, na kwamba atapunguza tatizo la uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi katika Shule za Sekondari.

” Katika hili ni wazi kuwa tutasambaza Kompyuta na kutumia mwalimu mmoja kufundisha shule zote kwa njia ya mtandao, maana najua kuna upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi, sasa nataka kupunguza tatizo hilo,” Amefafanua Mavunde.

Changamoto ya uhaba wa Walimu wa masomo ya Sayansi umekua ukizikabili shule mbalimbali nchini, kitu ambacho kinapaswa kutofumbiwa macho kutokana na na mahitaji ya wahitimu wenye taaluma hiyo katika Dunia ya leo iliyopiga hatua kubwa ya kiteknolojia.

Hii Simba ya sasa inaweka rekodi tu
Faiza afunguka kwa mara ya kwanza kulizwa na harusi ya Sugu