Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana na Ajira), Anthony Mavunde amewataka vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kujiongezea kipato pamoja na kuongeza ujuzi.

Ameyasema hayo jijini Tanga wakati akizindua Program ya Urasimishaji Ujuzi kwa Vijana ambao wana ujuzi lakini hawakupitia katika mfumo rasmi wa mafunzo ya Ufundi (Recognition of Prior Learning).

Amesema kuwa serikali inatekeleza mpango mkubwa wa ukuzaji ujuzi kwa Vijana unaolenga kuwafikia takribani Vijana Milioni 4 nchi nzima kwa lengo la kuwajengea ujuzi stahiki utakaowasaidia kupata Ajira na kujiajiri wenyewe.

Aidha, Mavunde amewataka Vijana wote kuchangamkia fursa mbalimbali zitokanazo na ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima, Uganda-Tanga ambapo serikali kuu na serikali ya Mkoa wameendelea kujenga mazingira rafiki ya kuhakikisha Vijana wanafikia malengo yao.

Hata hivyo, Program hiyo ya Urasimishaji Ujuzi inagharamikiwa  na Ofisi ya Waziri Mkuu na kwa kuanza umewafikia vijana kutoka mikoa ya Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Manyara kisha vijana wa maeneo mengine watanufaika na mpango huo.

LIVE: Rais Magufuli akihutubia katika uzinduzi wa kiwanda cha dawa Mwanza
Zitto Kabwe akamatwa na jeshi la Polisi