Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameishauri Serikali kuangalia suala la riba kwa watanzania ambapo amesema kuwa riba kubwa imekuwa ikiwatesa na wao kushindwa kufanya biashara kutokana na ukubwa wa riba.

Mavunde ameyasema hayo leo Juni 15 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo amemshauri Waziri mwenye dhamana kuangalia swala ili ili lisiwe kikwazo kwa watanzania.

Amesema watanzania wengi hawawezi kukopa katika mabenki nchini kwa riba ya kati ya asilimia 21 hadi 22.

“Riba inawaumiza hasa walimu wengi utakuta makochi na TV zao zimechukuliwa, tunawatesa sana watanzania,”amesema Mavunde

Serikali yaja na mkakati wa kumlinda Mzee
Rais Samia awatumbua DC, DED Morogoro