Mkaguzi wa mamlaka ya uthibiti wa mbolea Tanzania TFRA Raymond Konga amewaasa mawakala wa usambazaji wa mbolea kwa wakulima nchini kuweka mbolea zenye ujazo wa aina mbalimbali ili wakulima waweze kupata mbolea na kuboresha kilimo.

Konga amesema mawakala wengi wa mbolea wanapenda kuuza mbolea zenye ujazo kuanzia kilogranu 25 mpaka 30 na kupelekea kuwa na changamoto kwa wakulima wadogo kushindwa kumudu gharama.

Amesema hayo kwenye maonyesho ya “NaneNane” kanda ya mashariki ya kati yanayofanyika katika viwanja vya mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo eneo la tungi nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro

Amewataka wakulima kutembelea maonyesho ya nanenane, kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo ikiwemo matumizi sahihi ya mbolea na kuleta tija kwenye kilimo.,

Naye afisa mauzo wa kampuni ya usambazaji pembejeo za kilimo EGT inputs Ltd ya mjini Morogoro Elisafi Mapunjo amewashauri wakulima wadogo wa mkoani hapo kuungana pamoja katika vikundi ili kuweza kuagiza mbolea ya kilo tano.

Mbeya City watuma salamu Simba, Young Africans
Namungo FC wakwama usajili wa Ajibu, Mobby

Comments

comments