Mawakili wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump wametoa hoja za kuipinga kesi dhidi ya mteja wao wakati wa ufunguzi wa mchakato wa kumtetea kiongozi huyo katika kesi ya kutaka ashtakiwe.
Tayari Maseneta wa chama cha Republican wameonesha kwamba watapiga kura ya kumuondolea lawama kiongozi huyo wa zamani wa Marekani katika mashtaka yanayohusiana na uchochezi wa vurugu.
Maseneta hao wamedai kwamba kesi hiyo iko kinyume na katiba na kwamba Trump hakuwachochea wafuasi kulivamia bunge la nchi hiyo,CapitolHill Januari 6. Siku ya Jumanne
Mawakili waandamizi wa Trump, Bruce Castro na David Schoen walikuwa katika hatari ya kuipoteza kura moja ya Seneta wa Republican baada ya seneta huyo Bill Caasidy kusema kwamba wamekosea sana kusema kwamba kesi hiyo ni kinyume na katiba.
Rais Joe Biden akizungumzia kesi hiyo jana alhamisi amesema ushahidi dhidi ya mtangulizi wake huyo una nguvu kiasi kwamba unaweza kuzibadili fikra za baadhi ya Maseneta.