Mawakili wanaomtetea Rais wa Marekani, Donald Trump katika sakata la Urusi kuingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani ambayo inatuhumiwa kumsaidia Rais huyo, limechukua sura mpya mara baada ya msemaji wa mawakili hao kujiuzuru.
Mark Corallo ambaye alikuwa msemaji wa wakili Marc Kasowitz amejiuzuru mara baada ya kutofautia huku msemaji huyo akidai kuwa mawakili hao wamekuwa na dharau kubwa kwa msemaji huyo kiasi cha kumpunguzia ufanisi wake katika kazi.
Aidha, ameongeza kuwa amekatishwa tamaa na mawakili hao licha ya upinzani uliopo katika uchunguzi huo unaoendelea kuhusu tuhuma zinazomkabili Rais Doknald Trump wa Marekani.
Hata hivyo, wakili wa Idara ya Haki, Robert Mueller ambaye anaongoza uchunguzi huo, amemsifu kiongozi huyo kwa kuchukua maamuzi hayo huku akiajiri watu mashuhuri kuungana na timu yake ya uchunguzi