Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amewaonya na kuahidi kuwachukulia hatua kali mawakili wote wanaopotosha maamuzi ya mahakama kwa kukiuka maadili ya taaluma, kupitia mitandao ya kijamii.

Jaji Ibrahim ametoa kauli hiyo leo Desemba 21 katika hafla ya uapisho ya mawakili mapya 166, iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam ambapo amesema ofisi yake inapokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu ukiukwaji wa maadili unaofanywa na baadhi ya mawakili wasio waaminifu.

‘Kwa sasa changamoto ya ajira ni kubwa katika dunia ya ushindani duniani inakuwa kwa kasi teknolojia ukichukua nafasi hivyo mawakili hawana budi kupambana na changamoto hii,” amesema Prof Ibrahimu Juma.

Aidha, Jaji Mkuu amezungumzia changamoto kwa baadhi ya mawakili kutumia vibaya taaluma zao kwa kuchelewesha kesi kwa makusudi ili kuwapendelea wateja wao.

Kufuatia changamoto hiyo Profesa Ibrahim amewaasa mawakili wapya kuwa wabunifu kwa kuongeza ujuzi kuhusu taaluma zao ili wakidhi soko la ajira, na kuwataka kujiweka tayari kupambana na changamoto ya ajira katika karne ya 21.

Aweso aagiza ujenzi visima viwili Dodoma
Nandy, Dj Sinyorita, Rayvvan na Diamond Platnumz wangara tuzo za AEAUSA

Comments

comments