Baraza la Mawaziri la kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanategemea kukutana kesho Mei 28, 2021 Jijini Arusha kujadili masuala mbalimbali ya kukuza biashara na uwekezaji ndani ya Jumuiya hiyo. 

Mkutano huo wa Mawaziri umetanguliwa na mkutano wa Makatibu Wakuu wa sekta ya Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) wa Jumuiya hiyo uliofanyika leo Mei 27, 2021 jijini Arusha.

Aidha viongozi hao wamepokea na kujadili ripoti mbalimbali ikiwemo ripoti za baraza la kisekta la mawaziri wa fedha, ripoti ya kamati ya forodha, ripoti ya kamati ya biashara, ripoti ya kamati ya viwango ya Afrika Mashariki, ripoti juu ya masuala ya ushindani pamoja na ripoti ya kamati ya uwekezaji.

Mkutano wa Makatibu Wakuu wa leo tarehe 27 Mei 2021 utafuatiwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa kisekta tarehe 28 Mei 2021 jijini Arusha.

Kilio nyumba za ibada katikati ya makazi chamgusa RC Makalla
Rais Samia akutana na Rais wa Mahakama Afrika