Mawaziri wa fedha wa nchi saba tajiri G7 wanaanza Mkutano wa siku mbili mjini London kujadili njia za kufikia mkataba wa kimataifa juu ya kuongeza kodi kwa kampuni kubwa, ikiwa ni pamoja na kampuni za mitandao za Google, Facebook na Amazon.

Mkutano huo unaofanyika chini ya uenyekiti wa Waziri wa Fedha wa Uingereza Rishi Sunak, unawakutanisha Mawaziri hao wa Ujerumani, Ufaransa, Italia, Canada ana kwa ana kwa mara ya kwanza tangu kuzuka janga la corona.

Sunak ameelezea matumaini ya kupatikana makubaliano kwenye Mkutano huo, hasa kutokana na dhamira ya Rais wa Marekani Joe Biden ya kutaka kampuni kubwa duniani zitozwe kodi zaidi.

Hata hivyo, changamoto kubwa ni namna ya kufikia makubaliano juu ya kuleta mageuzi katika mfumo wa kodi, ambapo makubaliano hayo yatapaswa kuwasilishwa kwenye mkutano wa kundi la nchi za G20 utakaofanyika mwezi ujao nchini Italia.

Marekani imependekeza kiwango cha chini kuwa ni asilimia 15 kwa kampuni 100 kubwa kabisa duniani, na inatarajia makubaliano kamili kupatikana kwenye mkutano utakaohudhuriwa na Marais na Mawaziri Wakuu wa kundi la nchi wanachama wa G20 utakaofanyika nchini Uingereza kuanzia tarehe 11 hadi 13 mwezi huu.

Mfikirwa: Manji ruhsa kurudi Young Africans
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 4, 2021