Uongozi wa klabu bingwa nchini Italia Juventus FC, umepewa mtihani mzito na meneja wa kikosi cha klabu hiyo Max Allegri wa kuhakikisha wanampatia mkataba mpya kabla ya mwisho wa mwezi huu.
Allegri anaehusishwa na taarifa za kumrithi Arese Wenger huko kaskazini mwa London, ameweka msimamo huo kutokana na kuona hakuna purukushani zozote za kupatiwa mkataba mpya ambao utamuwezesha kufanya kazi klabuni hapo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye tovuti na Football Italia Allegri ameutaka uongozi wa klabu hiyo kumpatia mkataba wa miaka minne ambao utakua na thamani ya Pauni milioni 4.35 kwa mwaka .
Tivuti hiyo imeendelea kubainisha kuwa, meneja huyo pia ameutaka uongozi wa Juventus kumuachia madaraka ya kukiendesha kikosi cha kwanza kwa kufanya anachokitaka kwa ajili ya maendeleo.
Wakati huo huo fununu zingine zinadai kuwa, Allegri anatamani kujiunga na klabu ya Barcelona ambayo mwishoni mwa msimu huu itakua haina mtu wa benchi la ufundi kufuatia kuondoka kwa Luis Enrique.
Fununu hizo zimedai kuwa, Allegri anajipa matumaini makubwa ya kupatya kazi Camp Nou, tofauti na Emirates Sytadium yalipo makao makuu ya klabu ya Arsenal.