Aliyekua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Marcio Maximo amemtaja Fredrick Mwakalebela kama mbadala sahihi wa nafasi ya urais wa shirikisho la soka nchini TFF.
Kocha huyo kutoka nchini Brazil amempendekeza Mwakalebela kabla ya saa 24 kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF ambao utafanyika mjini Dodoma.
Maximo ameonekana akitoa mapendekezo hayo kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF wenye ridhaa ya kumchagua rais mpya wa TFF pamoja na safu ya kamati ya utendaji, kwa njia ya Video.
Katika Video hiyo, Maximo amesikika akisema “Binafsi rais anayestaili kwa hivi sasa TFF ni Mwakalebela pekee kutokana na utendaji wake kazi.
“Nakumbuka Mwakalebela alikuwa katibu kipindi cha rais Tenga (Leodegar) ambaye ni rais bora kabisa aliyeweza kuliongoza vyema shirikisho la soka Tanzania.
“Hivyo, kutokana na ubora huo wa Tenga ninaamini Mwakalebela atafuata utawala bora kupitia kwa Tenga aliyeweza kuliendelesha shirikisho hilo kwa mafanikio, hivyo ninawashauri wapiga kula wamchague Mwakalebela,” alisikika Maximo aliyewahi kuwanoa mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans.