Kocha mkuu wa timu ya Prisons, Salum Mayanga amesema ni ngumu sana kupata ushindi kwenye viwanja vya ugenini hivyo ushindi walioupata kwenye mechi yao ya jana dhidi ya Toto Africans walilazimika kuulinda mpaka mwisho wa mchezo.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu ilichezwa kwenye uwanja uwanja wa CCM Kirumba ambapo Prisons ya jijini Mbeya ilishinda bao 1-0, bao ambalo lilifungwa na Jeremia na kufanikiwa kuondoka na pointi tatu za ugenini.

“Kwa jinsi ligi ilivyo sasa hivi kupata ushindi wa ugenini ni shida sana, hivyo ukifanikiwa kufunga bao unatakiwa kulilinda mpaka mwisho ili wapinzani wasikuharibie mipango yako, ndiyo maana hata mimi niliamua kucheza kwa kupaki basi huku tukishambulia kwa kushitukiza tu,” alisema Mayanga.

Mayanga alisema kuwa timu ya Toto ambayo kwa sasa inafundishwa na mzungu, Dominic Glawogger  ni timu nzuri na si ya kuibeza, kwani uchezaji wao unaeleweka huku akidai wachezaji wao wanajituma wakionyesha nia ya kupata bao.

Kwa matokeo hayo Prison imefikisha pointi 24 huku Toto wao wakibaki na  pointi zao 17 ambapo kila mmoja amecheza mechi 14.

Ibrahim Ajib Awatoa Hofu Mashabiki Wa Simba
Hadji Mwinyi: Udhaifu Wa Oscar Joshua Ndio Mtaji Wangu