Kocha wa muda wa klabu ya Simba Mganda Jackson Mayanja ameanza kwa kasi majukumu ya kukinoa kikosi hicho kwa kuwakimbiza wachezaji wake, huku akitaja uwezo wa chini wa hali ya ufiti wa wachezaji wake ndiyo jambo atakaloanza nalo.

Akizungumza mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi katika Uwanja wa Amaan Mayanja alisema, Simba aliyoikuta isingeweza kupata matokeo yaliyokuwa yakihitajika katika hali ya ufiti wa wachezaji aliyoikuta ambayo haiendani na ukubwa wa timu hiyo.

Kiungo huyo wa zamani wa KCC ya Uganda alisema hilo ni jukumu lake la kwanza aliloanza nalo lakini akawataka wanasimba kumpa muda na kuwa wavumilivu wakati huu akibadilisha baadhi ya mambo katika kikosi chao hicho.

Alisema amewataka wachezaji wake kuwa tayari kupokea mazoezi yake na kwa haraka ameridhika na viwango vya wachezaji akisema kila kitu kitaenda sawa kama watashikamana.

“Simba ina hadhi yake hii ni timu kubwa sasa hata kiwango chake kiwe ni kile kinachosubiriwa na mashabiki na viongozi wao, kuna mambo yalipungua hapa sitaki kuzungumza sana tutafanya marekebisho mengi mazoezini sio katika vyombo vya habari,”alisema Mayanja.

“Wito wangu kwa Wanasimba wasiikimbie timu yao sasa warudi tushikamane lakini pia wawe na subira kidogo wakati huu tunabadilisha mambo hapa haya yanahitaji muda kidogo hatuwezi kupata matokeo wakati vifua vya wachezaji vikiwa vyepesi.

Watoto Wa Azam FC Wawafundisha Soka Wanajeshi
Penzi la Mrembo huyu lilikuwa chambo ya kumkamata Bilionea wa Unga 'El Chapo', Meseji zao ziko hapa