Mjumbe wa Kamati Kuu ya ufundi ya shirikisho la kandanda hapa nchini Tanzania TFF, Ally Mayay amesema kuwa anatarajia kufanya mabadiliko makubwa ndani ya shirikisho hilo.

Ameyasema mara baada ya Kamati hiyo kupanga kukutana siku chache zijazo ili kujadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuendeleza soka la hapa nchini Tanzania

Mjumbe huyo pia alikuwa mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya Urais katika shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, amesema kuwa tangu kamati hiyo itangazwe bado wahusika hawajakutana na kujadili mipango yao.

Mayay ambaye ni nyota wa zamani wa klabu ya CDA ya Dodoma,Yanga ya Dar es salaam na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars amesema kuwa kamati yao ina majukumu makubwa sana katika soka la Tanzania hivyo wana kila sababu ya kuhakikisha wanapitia mapendekezo kabla ya kuyapeleka katika sekretarieti itakayokua na maamuzi ya juu zaidi

“Tunapozungumzia kamati ya ufundi tunamaanisha masuala ya  ufundi wote wa kimichezo, wachezaji marefa, madaktari kwa hiyo tunajadili jinsi ya kuboresha utendaji,” amesema Mayay

Hata hivyo, Kamati ya Ufundi iliyoteuliwa na Rais mpya wa TFF, Wallace Karia ambapo alimtaja Mwenyekiti wa kamati hiyo kuwa Vedastus Lufano, Makamu Mwenyekiti ni Issa Bukuku na wajumbe ni Sarah Chao, Ally Mayay, Michael Bundala, Omar Abdulkadir na Israel Mujuni.

Tundu Lissu anayo mengi ya kuzungumza- Nape Nnauye
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 9, 2017