Nyota wa zamani wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Ally Mayay Tembele amechukua fomu za kuwania Urais wa TFF.

Mayay ametumia haki yake kikatiba kwa kufika ofisi za TFF mapema leo mchana akiambatana na mdau mwenzake Dominic Salamba.

Hii ni mara ya pili kwa Ally Mayay kuwania nafasi ya Urais wa TFF, mara ya kwanza ilikua mwaka 2017 ambapo aliangushwa na Rais wa sasa Wallace Karia.

Kuchukua fomu kwa mdau huyo ambaye pia hupenda kulichambua soka la Bongo kupitia Azam TV na vyombo vingine vya habari nchini kunaongeza idadi ya wanaowania kiti cha Urais wa TFF.

Kabla ya Mayay waliokua wamechukua fomu za kuwania kiti cha Urais ni Wallace Karia, Deogratius Mutungi, Evans G. Mgeusa, Zahoro M. Hajji na Oscar Oscar.

Uchaguzi Mkuu wa TFF umepangwa kufanyika mapema mwezi Agosti jijini Tanga.

Bodaboda, bajaji faini sh 10,000
TBS yaagiza mtambo wa Bil 3