Wakati timu ya Yanga ikipitwa pointi nane na watani zao Simba kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, mshambuliaji wa Yanga, Maybin Kalengo amesema kwamba wao hawashindani na watani zao  Simba .

Kalengo huyo aliyetua Yanga akitokea kwa mkopo Zesco United ya Zambia ameweka wazi hilo wakati ambao Yanga wapo nafasi 14 kwenye msimamo wakiwa na pointi nne huku Simba wakiwa kileleni na pointi 12.

Mshambuliaji huyo amesema kuwa wao hawashindani na Simba hata kidogo kutokana na kujiwekea malengo ya kupambana na timu zote za ligi na kutwaa pointi tatu kila watakapokutana nao.

“Kwa sasa hatuwezi kuwaahidi sana mashabiki zetu kwamba tutafanya nini kwa sababu ndiyo ligi iko mwanzoni lakini kitu kikubwa tutakachofanya ni kupambana, “amesema Kalengo.

Video: Rugemalira aamsha upya mzimu wa Escrow, Nyerere Hajafa
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 11, 2019