Klabu ya Young Africans imeendelea kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kufuatia kuichaoa Geita Gold bao 1-0 kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Fiston Mayele ameendelea kuwatesa makipa wa ligi kuu ambapo leo tena kaweka kambani goli la pekee lililowapa alama tatu muhimu kwenye ligi hiyo.

Mayele alifunga bao la mapema kabisa baada ya kuwashinda mabeki wa Geita Gold na kuweza kufyatua shuti kali lililomshinda kipa wa Geita Gold Aron Kalambo.

Mchezo huo ambao ulikumbwa na faulo nyingi kwa pande zote mbili na kusababisha wachezaji baadhi kutolewa nje kwa majeruhi.

Simba, Dodoma Jiji zapokea taarifa ya TPLB
Polisi kukomesha mauaji Tabora