Mshambulaiji wa Young Africans Fiston Kalala Mayele ametoa ufafanuzi wa aina ya ushangiliaji alioutumia katika mchezo wa jana Alhamis (Novemba 17), walipocheza dhidi ya Singida Big Stars kutoka mkoani Singida.
Mshambuliaji huyo kutoka DR Congo alifunga mabao matatu pakee yake ‘HAT TRICK’, huku bao lingine likifungwa na Beki wa Kulia Shomari Kibwana na kuifanya Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.
Mayele alishangilia kwa ishara ya kubebelaza mtoto alipofunga bao la kwanza na la nne katika mchezo huo, na kuibuka sintofahamu kwa baadhi ya Mashabiki ambao walimzoea kwa ushangilia wa Kutetema.
Alipohojiwa na Azam TV baada ya mchezo huo kumalizika, Mayele alisema alishangilia kwa ishara ya kubembeleza mtoto kama zawadi kwa Mwanaye wa Kike aliyezaliwa Jumanne (Novemba 16).
“Kweli tumepata mtoto watatu ni wa Kike alizaliwa Juzi (Jumanne) anaitwa Makhael, Goli la kwanza nimemzawadia Mwanangu.” alisema Mayele
Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa Young Africans mwanzoni mwa msimu uliopita amefikisha mabao Sita msimu huu, akimfikia Mshambuliaji wa Simba SC Moses Phiri, huku Sixtus Sabilo akiwa kileleni kwa kupachikwa mabao Saba.