Mshambuliaji wa zamani wa Young Africans, Fiston Mayele, amesema kwa namna anavyomfahamu Maxi Nzengeli, anaamini nyota huyo ataisaidia sana timu hiyo kutetea ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2023/24.

Mayele ambaye aliitumikia Young Africans kwa misimu miwili, ameondoka kikosi hapo hivi karibuni na kutua Pyramids ya Misri, huku Nzengeli akiwa ni usajili mpya ndani ya Young Africans. Nyota hao wote ni raia wa DR Congo.

Mayele ameweka wazi kuwa, anamfahamu vizuri Maxi, hivyo hana hofu na msaada wake ndani ya Young Africans, anaamini kama ataendelea kupewa nafasi basi ataibeba zaidi timu hiyo.

“Maxi ni kati ya wachezaji wenye uwezo mzuri sana wa kufunga, hivyo sina shaka na alichoanza kukionesha, kikubwa anahitaji nafasi tu ya kucheza zaidi ya hapo,” amesema.

Maxi msimu huu katika michuano yote ambayo Yanga imecheza, tayari amefunga mabao manne, mawili Ligi ya Mabingwa Afrika na mengine Ligi Kuu Bara.

Viongozi wa Afrika wahimizwa kuwa na kauli moja
Waliotega vilipuzi vya kienyeji Kanisani wadakwa