Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Mayele, ametamba kuendelea kupambana ili kuiwezesha Young Africans kupata alama tatu muhimu dhidi ya Mtibwa Sugar, kesho Jumatano (Februari 23).

Mtibwa Sugar watakua nyumbani Manungu Complex wakiikaribisha Young Africans kwenye mchezo wa Mzunguuko wa 15 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mayele amesema licha ya kufahamu kuwa mchezo huo utakuwa mgumu lakini watapambana kama timu kuhakikisha wanaibuka na ushindi muhimu, kutokana na kufahamu umuhimu wa mchezo wenyewe.

“Tunafahamu ukubwa wa mchezo huu, ni mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi, hivyo tunatakiwa kuumaliza kwa ushindi, naona utakuwa mchezo mgumu kwa kuwa tutakuwa ugenini lakini hatuhofii hilo.”

“Sisi tupo tayari kwa ajili ya mapambano na tutapambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha tunaondoka na ushindi, kila mchezo kwetu unahitaji ushindi, na hiyo ni kutokana na kuhitaji kutimiza malengo yetu msimu huu,” amesema Mayele.

Young Africans inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 36, huku Mtibwa Sugar ikisota katika nafasi 15 ikiwa na alama 12.

Simba SC yamuwinda Arno Buitenweg
Simba SC kuendelea na safari ya Morocco leo