Bingwa wa zamani wa dunia wa masumbwi, Floyd Mayweather amefunga mjadala wa kuwepo pambano la marudiano kati yake na Conor McGregory kwa kufuata kanuni za MMA, UFC kwa kutumia ngumi, mateke viwiko n.k.
Bondia huyo ambaye Jumamosi hii alienda kushuhudia mechi ya mpira wa kikapu ya ‘NBA All Stars’, alimwambia mwandishi wa habari kuwa hana mpango wa kupigana tena na McGregory kwakuwa alimpiga tayari.
“Nilishapigana na Conor na nikampiga. Na hapa tuko kwenye mechi ya mpira wa kikapu na sio kwenye MMA,” alimjibu mwandishi huyo aliyebobea kwenye habari za MMA.
Muda mfupi baada ya majibu hayo ya Mayweather kuanza kusambaa, McGregory alimjibu kupitia Instagram akimtakia kila la kheri kwa kujiweka kando na pambano dhidi yake, hasa kupitia MMA, UFC.
McGregory ambaye ni bingwa wa mapigano ya UFC ya ngumi na mateke aliyeamua kumkabili Mayweather kwenye pambano la masumbwi na kupigwa ‘KO’, alisema anaachana rasmi na Mayweather na kumtafuta mpiganaji mwingine. ]
“Ninamuelewa sana kwa kuamua kustaafu. Sasa nitaendelea na mazungumzo na mpiganaji mwingine kabisa. Kuwa na kustaafu kwema Jonior,” unasomeka sahemu ya ujumbe wa McGregory.
Pambano la Mayweather na McGregory linatajwa kuvunja rekodi ya mapambano yote ya ngumi kwa upande wa mauzo.