Bondia Floyd Mayweather ameutolea uvivu muziki wa rap na wasanii wanaojihusisha na muziki huo hivi sasa akidai kuwa wanahalalisha matumizi ya dawa za kulevya na wanaishi maisha feki.

Bingwa huyo wa zamani wa dunia ambaye hajawahi kushindwa pambano hadi alipoamua kustaafu, amefunguka katika mahojiano aliyofanya Jumanne hii na Whoolywood Shuffle, bila kujali ukaribu wake na wasanii wa hip hop.

“Huu ni ukichaa, eti sasa hivi ni sawa tu kutumia dawa yoyote ya kulevya, ni sawa tu kuwa teja,” alisema Mayweather kwa mshangao.

Katika hatua nyingine, aliwalinganisha wasanii nguli wa zamani na walivyo wasanii wanaotamba hivi sasa. Alisema wakali kama 2 Pac na Biggie walikuwa wanaishi wanachokiimba na muziki wao ulikuwa hauipitwi na wakati tofauti na wanachofanya marapa wa sasa.

“Magwiji na nguli wa rap walipenda kusimamia kile wanachokizungumzia. Ukirudi nyuma na kusikiliza nyimbo za nguli hao wa rap, ni muziki ambao haupitwi na wakati. Watu kama Biggie, kama Pac, muziki wa muda wote haupitwi na wakati,” alisema.

Ingawa hakutaja majina ya marapa anaowachana, ni rahisi kwa wafuatiliaji wa mambo kuhisia anaowazungumzia kwa kuzingatia baadhi ya maandishi yake ya hivi karibuni kwenye mitandao na jinsi alivyokuwa karibu na wasanii wakubwa ambao wamewahi kusikika wakiimba mistari inayosifia dawa za kulevya aina ya Lean na Molly.

August Alsina aweka wazi ugonjwa wa ini unavyomtesa
Video: Msifanye kazi kwa kutafuta kiki na sifa-Lema