Jarida maarufu la Forbes limetoa orodha mpya ya wanamichezo ambao wanalipwa pesa nyingi, orodha hiyo ikijumuisha kipato kilichoingizwa na wanamichezo husika kutokea mwaka jana mwezi Juni 2017 hadi Juni 2018.
Mwanamasumbwi kutoka Marekani Floyd Mayweather mwenye umri wa maiaka 41 ameendelea kushika namba moja katika orodha hiyo akiwa ametengeza kiasi cha dola za Kimarekani milioni 285.
Pambano kati ya Meyweather na Conor McGregor lililopigwa mwaka jana ndilo lililompatia kiasi kikubwa cha pesa Mayweather ambapo aliingiza kiasi cha milioni 275 dola za kimarekani.
Nyota wawili wa soka Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndio wanaomfuatia Mayweather, ambapo Messi yuko nafasi ya pili akiwa amelipwa dola milioni111 huku Ronaldo akiwa amelipwa kaiasi cha dola milioni 108.
Bondia Conor McGregor anashikilia nafasi ya nne akiwa na dola milioni 99m huku mchezaji ghali zaidi duniani Neymar akiwa katika nafasi ya 5 na kiasi cha dola milioni 90.
Nafasi ya sita yupo LeBron James na kiasi cha dola milioni 85.5 huku mcheza tennis Rodger Federer akiwa nafasi ya saba na dola miloni 77.2, Stephen Curry yuko nafasi ya nane na dola miloni 76.9, nafasi ya 9 ni mchezaji wa baseball Matt Ryan aliyeingiza dola za kimarekani milioni 67.3 na nafasi ya 10 ni Matthew Stafford aliyelipwa kaiasi cha dola milioni 59.5.
-
Mjue Mtanzania atakayecheza kombe la Dunia mwaka huu Urusi
-
Hector Cuper atoa somo la saikologia kwa wachezaji wa Misri