Bondia Floyd Mayweather ambaye ametangaza kurejea tena ulingoni kumvaa Manny Pacquiao, amejiongeza pambano moja la ziada kabla ya pambano hilo.

Mayweather alikubali kupigana tena na Pacquiao walipokutana wikendi iliyopita katika tamasha la muziki jijini Tokyo nchini Japan, akitaja Disemba kuwa mwezi wa pambano la marudiano.

Hata hivyo, watu wa karibu wa Mayweather wameuambia mtandao wa TMZ kuwa Mayweather atapambana na bondia mmoja nchini Tokyo, kama pambano la kurejea lakini hakumtaja bondia huyo.

Imeelezwa kuwa hadi sasa Mayweather hajachagua bondia wa kupigana naye kabla ya pambano lake na Pacquiao, lakini inadaiwa kuwa anafanya hivyo kwa malengo ya kibiashara kuteka soko la Japan na bara la Asia.

Inadaiwa kuwa ingawa Pacquiao na Mayweather ambao wote wanamiliki makampuni yao binafsi ya promotion (Pacman Promotion na Mayweather Promotion), wanaweza kuichagua Disemba 31 kuwa siku ya pambano hilo.

Hata hivyo, bado hawajafanya makubaliano rasmi kati yao hivyo chochote kinaweza kutokea wakati watakapoanza makubaliano.

Mayweather alimshinda Pacquiao kwenye pambano lao la raundi 12 lililofanyika Mei 2015 nchini Marekani.

Mayweather (50-0) mwenye umri wa miaka 41, anarejea ulingoni wakati ambapo Pacquiao (60-7-2) mwenye umri wa miaka 38 anatarajia kupigana mapambano mawili zaidi kabla ya kutundika ‘gloves’.

Video: Soudy Brown, Maua Sama wasota rumande, Chadema hawaaminiki
Nandy afunguka collabo yake na msanii wa Marekani, 'Rihanna!?'