Eva Godwin – Dodoma.

Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ibenzi Ernest amesema Mazingira ya Hospital hiyo yaliyojaa nakshi za maua na usafi wa maeneo, yamekuwa yakiwavutia Maharusi kufungia pingu za maisha.

Dkt. Ibenzi ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma, na kudai kuwa Hospitali hiyo imekuwa ni kivutio kwa Watu wengi ambao wanafika mahali hapo.

Amesema, “Hospitali hii imekuwa ya kipekee sana Dodoma na inashangaza mpaka Maharusi wanaomba kuja kupiga picha za ndoa katika mazingira ya hospitali yetu, hii imewavuta watu wengi Mkoani hapa na nje ya Mkoa.”

Hata hivyo, Dkt. Ibenzi amesema Hospitali kwa mwaka jana ilikuwa ya kwanza Kidunia kutibu Magonjwa ya mifupa na kusema, “hii imetupa nguvu ya kuendelea kupiga hatua kubwa zaidi na kupitia hiyo sifa, Serikali itumeongezea vifaa vya kutosha katika kutibu magonjwa ya mifupa pamoja na magonjwa mengine.”

Aidha, ameongezea kuwa hivi karibuni mirundikano kwa wodi ya Watoto itapungua kutokana na wodi mpya inayojengwa kukaribia kukamilika hivi karibuni baada ya kupata malalamiko hayo ambayo yamefanyiwa kazi na ufumbuzi kupatikana.

Mkuu Shule ya Polisi Moshi autaka ubingwa ligi Kuu
Maisha: Uamuzi wako umebeba hatma ya wengine