Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amekutana na watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati jijini Dodoma leo Juni 14, 2023.
Akizungumza na watumishi hao amewahimiza waendelee kufanya kazi kwa kujituma ili kuisaidia Serikali katika jitihada zake za kuhakikisha Sheria ya Mazingira inatekelezwa ipasavyo na kutoa wito kwa watumishi hao wawe na moyo wa kuipenda kazi yao na kuleta tija kwa taasisi, Serikali na jamii kwa ujumla ili kuleta matokeo mazuri.
Amesema, “ndugu zangu niwaambie unapokuwa kazini kitu cha muhimu uache legacy na hata wakati ukiwa likizo wenzako washtuke sio wakuulize sio unanda likizo na hakuna anayekuulizia, mahali pa kazi pia ni sehemu ya kuendelea kujifunza maarifa na mbinu mbalimbali za utendaji hivyo watumie kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha thamani ya kazi inaonekana.
Aidha, ametumia nafasi hiyo kuwatia moyo katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo operesheni ya kutokomeza mifuko na vifungashio vya plastiki vilivyopigwa marufuku na Serikali ambayo inaendelea kufanyika nchi nzima.