Utafiti ulifanywa na Dkt. Nizami Duran, Mkuu wa Idara ya Mikrobiolojia katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Hatay Mustafa Kemal umebaini kwamba Maziwa ya Mtindi ni kinga dhidi ya Homa ya Mafua.
Utafiti huo umeonesha mtindi huongeza kiwango cha ‘Immunoglobulin’ au ‘Antibody’ kwa kiwango kikubwa ambavyo ni kati ya vitu muhimu katika kuzalisha Kinga ya mwili dhidi ya magonjwa ya kuambukiza.
Katika utafiti huo wanyama walijaribiwa kwa kupewa mtindi na waliweza kutengeneza ‘Antibody’ mara 2 hadi 10 zaidi ukilinganisha na wale ambao hawakupewa.
Hali kadhalika wanyama hao waliopewa mtindi, kinga yao dhidi ya Magonjwa ya Mfumo wa Kupumua na haswa mafua iliongezeka kwa mara 10 zaidi.