Jamii imeaswa kuwa na desturi ya kufanya mazoezi mara kwa mara, kwani yana faida kubwa katika kuimarisha afya ya akili na afya ya mwili, ikiwemo kuzuia magonjwa yasiyoambukiza.

Hayo yamebainishwa  Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga, Wizara ya Afya Dkt. Khalid Massa katika Utekelezaji wa Mpango wa Mazoezi na Afya ya Mwili kwa watumishi ndani ya Idara ya Kinga.

Amesema, “tumeanza mazoezi haya ili kuhamasisha katika kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, mazoezi yana umuhimu sana si tu afya ya mwili bali afya afya ya akili na yanaongeza performance kubwa katika utendaji wa kazi”amesema.

Kwa upande wao baadhi ya Watumishi walio chini ya Idara ya Kinga, Wizara ya Afya wamesema mazoezi hayo ni muhimu kuimarisha afya zao na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi.

Idara ya Kinga Wizara ya Afya, imeanzisha Mpango kwa watumishi kufanya mazoezi mara mbili kwa wiki Jumatano na Ijumaa jioni mara baada ya saa za kazi ili kuungana na mkakati endelevu wa Wizara ya Afya wa Kupambana na Magonjwa Yasiyoambukiza.

Jando, Unyago mtaji kurekebisha tabia za Vijana
Namungo FC yaiwahi Young Africans Dar