Rais wa Marekani Donald Trump amerekodiwa akimwambia Kamishna wa uchaguzi katika jimbo la Georgia Brad Raffensperger,  kumtafutia kura 11,780, ambazo zingeweza kubadilisha matokeo na kumpokonya ushindi Rais mteule Joe Biden katika jimbo hilo la Kusini Mashariki.

Gazeti la Washington Post limeripoti na kutoa kanda ya sauti mazungumzo kati ya Rais Trump na Brad Raffensperger.

Katika mazungumzo hayo, Raffensperger na wakili wake wanasikika wakimfahamisha Trump kwamba madai yake kuwa amelishinda jimbo la Georgia yana msingi katika nadharia za uzushi ambazo zimethibitishwa kuwa za uongo, na kumhakikishia kuwa kura 11,779 ambazo Biden amemzidi Trump zilikuwa halali.

Kuchapishwa kwa mazungumzo hayo na gazeti la Washington Post ni ufichuzi wa juhudi nyingine ambazo Trump amekuwa akizifanya kwa miezi miwili iliyopita, kutaka kuwaaminisha watu kuwa kushindwa kwake na Joe Biden kulitokana na hila za wizi wa kura.

Madai hayo ya udanganyifu katika uchaguzi ambayo yanaendelezwa na Rais Donald Trump na washirika wake yametupiliwa mbali na maafisa wa uchaguzi wa majimbo na kesi zao nyingi zimetupwa nje na mahakama.

Pelosi achaguliwa tena Uspika Bunge la Marekani
CAF waridhia ombi la Simba SC