Ikitokea akaondoka Kylian Mbappe atakuwa hana lawama na klabu yake ya PSG kwa kuwa alishatoa taarifa mapema kuwa hataongeza mkataba mwingine klabuni hapo.

Mbappe alichosema kwa sasa anataka kusalia Paris Saint-Germain lakini anasema hataongeza mkataba wake zaidi ya 2024.

Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 unaisha mwishoni mwa msimu ujao huku kukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mwingine lakini yeye mawazo yake yamebadilika na hataki tena kubaki.

Jumanne wiki hii, nyota huyo alituma ujumbe kwenye Twitter kwamba ataendelea kubaki PSG, lakini barua kutoka kambi yake ilisema msimu ujao utakuwa wa mwisho katika klabu hiyo.

Mbappe anasema PSG waliambiwa kwa mara ya kwanza Julai 15, 2022 kuhusu uamuzi wake wa kukataa ya mkataba wa mwaka mmoja.

Hata hivyo, PSG wako tayari kumuuza mfungaji wao bora msimu huu kuepuka kumpoteza bure mwakani.

Mbappe alisema taarifa zinazodai anataka kujiunga na Real Madrid msimu huu wa joto ni uongo.

Polisi wakamata mamia ya mifugo, watuhumiwa 153 mbaroni
Bangala kumfuata Nassredine Nabi