Mshambuliaji Kylian Mbappe, anatarajiwa kukaa nje ya dimba kwa muda baada ya kupata majeraha ya Kifundo cha Mguu ‘ENKA’.
Mbappe alilazimika kutolewa nje katika mchezo Ligi ya Ufaransa mwishoni mwa juma lililopita kati ya Paris Sait-Germain dhidi ya Marseille, ambapo PSG ilibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Mbappe alipata majeraha ya enka wakati akipambana na Leonardo Balerdi kuwania mpira katika mchezo huo.
Staa huyo raia wa Ufaransa, pia hatakuwepo katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Newcastle utakaochezwa Jumatano (Oktoba 4).
Katika mchezo huo, mabao ya PSG yaliwekwa kimiani na wachezaji Achraf Hakimi, Randal Kolo Muani na Goncalo Ramos aliyefunga mawili.
Taarifa ilyotoka katika mtandao klabu hiyo kuwa Mbappe atakaa nje ya dimba kwa muda, kufuatia kupata majeraha ya enka.
“Mbappe hatakuwepo katika mechi kutokana na kupata majeraha ya tayari ameshaanza kupatiwa matibabu,” imeeleza taarifa hiyo.