Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema wananchi wanaotumia daraja la Tanzanite hawatatozwa fedha ya aina yoyoye

Mbarawa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 3, 2022 alipotembelea ujenzi wa daraja la Changombe jijini Dar es Salaam kufuatia kuwepo kwa maswali kwa nini daraja la Kigambo wananchi wanalipishwa tofauti na Tanzanite.

Amesema fedha zilizotumika kujenga daraja la Tanzanite ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Korea Kusini ambazo zitalipwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia zote.

Amesema hii ndio sababu ya wananchi wanaotumia daraja hilo kutolipishwa fedha kama inavyofanyika kwenye daraja la Kigamboni.

TACAIDS yateta na waandishi wa Habari
Waziri wa Utamaduni kukutana na wasanii